Ni muda mrefu tangu nilipoandika ripoti za huku kwetu, Somalia. Vita vimekuwa vikiendelea kwa muda mrefu, na watu wengi wamepata majeraha mabaya kutokana na viya hivyo. Wakenya waliokuja kutusaidia wamefanya kila juhudi ili waweze kutuokoa dhidi ya mikono ya wanakundi haramu la Al-Shabab.
Kwa wakati huu, watu wengi wamekombolewa, na miji mengi ambayo yalinyakuliwa na wanakundi hili yamerejehwa kwenye mikono ya serikali yetu. Kuna nchi zingine za Magharibi ambayo yanachangia kuvuruhika kwa amani kwetu. Walitaka nchi yetu ibaki nyuma milele, lakini nawapa mikono ya pongezi kwa ndugu zetu wakenya ambao waliweza kutusaidia.
Sasa, nimewasiliana na Bi O ili aweze kupanga pamoja na Benedict ili waweze kuniletea mbolea huku. Kuna wale ambao wamegundua kwamba ni mbolea ambayo yamekomboa nchi, kwa hivyo wanaitaka kwa njia yoyote iwezekanavyo. Hivi ni kumaanisha kwamba hivi karibuni naenda kuanza kusambaza Orgonite kwanjia vile tulivyo fanya na Benedict.
Fatuma










